Taarifa ya Kiikolojia ya Msitu wa Magombera

Research output: Book/ReportCommissioned report

Full text download(s)

Author(s)

Department/unit(s)

Publication details

DatePublished - 2008
Number of pages69
PublisherWorldwide Fund For Nature Tanzania Programme Office
Place of PublicationDar es Salaam
Original languageOther

Abstract

Muhutasari Mkuu

Maelezo ya Awali

Msitu wa Magombera ni eneo la misitu ya kitropiki ya nyanda za chini lililo katika tishio la kutoweka, lililojulikana kitambo kwa thamani kubwa ya bioanuai. Kati ya misitu yaTanzania ulijulikana kwa sababu ya savei za mwanzo na historia tata ya usimamizi wake. Savei ya kwanza ya kina ya mimea na wanyama pekee ilipelekea mamlaka zote za usimamizi kukubali kuwa eneo hilo liunganishwe katika pori la akiba la Selous lililo jirani. Hata hivyo baada ya kubadilisha umiliki wa Idara kuu ya misitu na nyuki mwaka 1981, mchakato wa kuunganishwa katika pori la akiba la Selous haukukamilika na hivyo kuacha msitu pasipo hadhi madhubuti ya ulinzi.

Hadhi hii ya kutolindwa vyema kwa msitu wa Magombera ilisisitizwa katika warsha ya mwaka 2004 iliyojadili vipaumbele katika milima ya Udzungwa na maeneo jirani yake. Hii ilifuatia matishio ya uharibifu ya kupatiwa eneo watu waliokaa kiharamu katika mashamba ya miwa yaliyo jirani na dukuduku kutoka katika jamii ya wahifadhi mazingira kitaifa na kimataifa, ikijumuisha Mheshimiwa waziri wa maliasili na utalii na mkuu wa shirika la ‘Conservation International.’ Kutoka katika warsha hii mipango iliwekwa ili kuanzisha mradi mpya wa uhifadhi chini ya ofisi ya programu Tanzania ya WWF.

Katika taarifa hii matokeo ya utafiti wa kiikolojia wa mradi mpya yanawasilishwa, pamoja na takwimu zilizokusanywa mwaka 2003-5. Matokeo haya yana ziada ya maelezo toka katika maandiko/machapisho mengine ya tafiti mbalimbali.


Lengo na Dhumuni

Kutokana na kuongezeka kwa utafiti kwa mika kumi iliyopita, sasa tuna taarifa za kutumainiwa za ikolojia ya msitu wa Magombera ikilinganishwa na misitu mingine Tanzania. Lengo la taarifa hii ni kutoa nguvu ya hoja ya uboreshaji usimamizi na ufuatiliaji wa kiikolojia wa msitu wa Magombera. Kuna makusudio makuu saba:

1) Kujulisha njia za kitafiti na matokeo ya savei mbili za kiikolojia;
2) Kutambua umuhimu wa kiikolojia wa msitu wa Magombera;
3) Kuweka kipaumbele katika matishio;
4) Kuangalia afya ya msitu;
5) Kuangalia hadhi ya spishi chache adimu na viashiria;
6) Kujaribisha njia za kurejesha msitu katika hali yake ya asili;
7) Kutoa mapendekezo kwa usimamizi, maisha ya jamii na ufuatiliaji kwa wakati ujao.

Discover related content

Find related publications, people, projects, datasets and more using interactive charts.

View graph of relations